Full-Width Version (true/false)


Afisa elimu manispaa ya Morogoro azindua majilisi "Vimbweta" 45 chuo kikuu cha waislamu Morogoro

 

 
Afisa elimu shule za msingi Manispaaa ya Morogoro, Abdul Bukheti amezindua "Majilisi"
maarufu kama vimbweta 45 katika chuo Kikuu Cha Waaislamu Morogoro vilivyotengenezwa kwa nguvu ya wanafunzi na msaada kutoka utawala.
 
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo ulifanyika leo Juni 1,2018 baada ya swala ya Ijumaa katika msikiti uliopo chuoni hapo, Bukheti ameipongeza serikali ya wanafunzi kwa kusimaamia zoezi la utengenezaji wa Vimbweta hivyo pia amewataka wanafunzi kuvitunza.
 
Abdul Bukheti,Afisa elimu shule za msingi Manispaaa ya Morogoro
 
Awali wakati anatoa taarifa ya utengenezwaji wa vimbweta hivyo, Rais mstaafu wa chuo hicho ambaye serikali yake iliaanzisha zoezi la utengenezaji ,Yahaaya Jameh ameeleza kuwa Vimbweta hivyo 45 vimegharimu Tsh 9,931,000 ambayo ilipatikana kwa harambee iliyoanzishwa  Janurai 19 mwaka huu msikitini hapo, pesa nyingine ilipatikana kutoka kwenye uogozi wa chuo. 
 
 Baadhi ya wanafunzi na wafanyakazi  wa chuo waliohudhuria kwenye uzinduzi huo

Nae Rais wa sasa chuoni hapo , Shabir  Birigwa amesema vimbweta hivyo vitasaidia katika kuhifadhi viti vya madarasani kwa sababu  vimbweta hivyo vitasaidia wanafunzi kufanya mijadala nje ya dararasa na viti kubaki ndani.
 
 Shabir  Birigwa,Rais MUMSO


PICHA NA SHABAN KIDIMILE-MOROGORO

 Abdul Bukheti na baadhi ya waalimu na wanafunzi wakiwa wamekaa kwenye vimbweta kuashiri uzinduzi

 Makamu  mkuu wa chuo,Prof Njozi (aliyekaa amevaa  kanzu nyeupe) pia alikuwepo kwenye uzinduzi huo uzinduzi ukiendelea

 Vimbweta vikiwa stoo Wanafunzi wameanza kuvitumia Vimbweta hivyo

No comments

Powered by Blogger.