Full-Width Version (true/false)


Ahadi za Wagombea Urais Zahojiwa Bungeni

Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Sophia Mwakagenda amehoji ni lini Serikali itazuia ahadi za wagombea urais  ambazo zinachukua muda mrefu kutekelezeka.

Sophia ameuliza swali hilo bungeni mjini Dodoma leo Alhamisi Juni 7, 2018, kuwa “Ni lini Serikali itazuia ahadi za wagombea urais ambazo wanatumia muda mrefu kuzitekeleza kama vile ujenzi wa barabara na zahanati.”

Akijibu swali hilo,  Naibu Waziri wa Tamisemi, Josephat Kandege amesema wagombea urais huenda kuuza sera na ilani za vyama vyao ili wachaguliwe na wananchi.

“Ilani ni mikataba ya miaka mitano hakuna sababu ya kuzuia kwasababu zimekuwa zikitekelezwa na mheshimiwa Naibu Spika wewe umekuwa shuhuda wa majibu yanayotolewa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM,”amesema.

No comments

Powered by Blogger.