Full-Width Version (true/false)


Akutana na Mama yake aliyemtupa akiwa mchanga, Kilichotokea !!

kisa kisicho cha kawaida kilishuhudiwa hivi majuzi baada ya mama kukutana na mtoto wake aliyetaka kumuua akiwa bado tumboni.


Mwaka wa 1977 mwanamke aliyekuwa na umri wa miaka 19 alitoa mimba kwa kutumia kemikali kwa zaidi ya siku tano na kupelekea mtoto kuzaliwa na kutupwa kwenye taka taka za hospitali.

Melissa Ohden, aliokolewa na mhudumu wa afya aliyemsikia akilia katika taka taka za hospitali nchini Marekani kabla ya kupata familia iliyomuasili.

Melissa ambaye ameandika vitabu kuhadithia maisha yake anasema aligundua kwamba aliasiliwa wakati alipogombana na dadake kutoka familia iliomuasili ndipo akaanza kumtafuta mamake mzazi akiwa na umri wa miaka 14.

Walipokutana ana kwa ana mamake alijutia kitendo hicho, kilichomsumbua roho kwa miaka mingi.

Kwa sasa Melissa na mamake mzazi wanaishi mjini Kansas pamoja na mojawapo wa dada zake wa kambo.

No comments

Powered by Blogger.