Full-Width Version (true/false)


Al-shabab Waua watu kwa kuwakata vichwa
Washambuliaji wa kundi la Al-shabab wameua watu saba kwa kuwakata vichwa vyao kwa mapanga na kuchoma nyumba zaidi ya 10 Kaskazini mwa Msumbiji. 

Jimbo la Cabo Delgado, ambalo linatarajiwa kugeuka kuwa makao makuu ya uzalishaji gesi asilia baada ya ugunduzi wa hivi karibuni kuonyesha matumaini, limekuwa likishuhudia mashambulizi ya mauaji dhidi ya vikosi vya usalama na raia tangu Oktoba mwaka jana.

Msemaji wa polisi Inacio Dina aliliambia shirika la AFP akirejea shambulizi la mwezi uliopita katika jimbo hilo, "Washambuliaji, Jumanne alfajiri, walichoma moto nyumba 164 na waliharibu magari manne walipofanya shambulizi katika kijiji cha Naude wilaya ya Macomia," amesema.

Washambuliaji ambao wenyeji na maofisa wanadai kuwa ni "al-Shabab", hawana uhusiano wowote na wale wa Somalia wanaotumia silaha na jina hilo hilo.

No comments

Powered by Blogger.