Full-Width Version (true/false)


''Alikiba anacheza mpira vizuri kuliko hata baadhi ya wachezaji wa Simba na Yanga' - Julio

Kocha  wa Dodoma FC Jamhuri Kihwelo maarufu 'Julio', amesema amekuwa akijitahidi kutaka kumsajili kwenye timu yake nyota wa muziki wa Bongofleva Alikiba kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kucheza soka kuliko wachezaji wa Simba na Yanga. 
Julio ameyasema hayo baada ya nyota huyo ambaye hivi karibuni ameachia ngoma yake mpya 'Mvumo wa Radi', kuonesha kiwango kikubwa kwenye mechi ya hisani maaalum kwa kuchangia fedha kwaajili ya wanafunzi wenye uhitaji iliyopigwa jana jioni kwenye uwanja wa taifa.

''Pamoja na mimi kuwa nilikuwa nafundisha timu ya Samatta lakini Alikiba binafsi namkubali sana na anajua kucheza, hata wachezaji wa timu kubwa kama Simba na Yanga hawana kiwango kama chake'', alisema Julio.

Julio ambaye anasifika kwa kuwa mwingi wa maneno ameongeza kuwa amekuwa akiongea na Alikiba ili amsajili kwaaajili kuchezea timu yake mechi za Dar es salaam kutokana na ratiba yake kumbana kwa mechi za mikoani lakini mfumo wa soka la Tanzania unamkwamisha.

Mchezo huo ambao ulikutanisha timu mbili zilizoundwa kwa pande mbili, timu ya marafiki wa Alikiba na timu ya marafiki wa Samatta, ilimalizika kwa timu ya Samatta kushinda mabao 4-2.

No comments

Powered by Blogger.