Full-Width Version (true/false)


Alikiba atangaza jeshi lake la kumvaa Samatta

 Mwanamuziki, Alikiba ametangaza kikosi chake kitakachocheza mchezo wa hisani utakaochezwa Jumamosi kati na marafiki zake na marafiki wa Mbwana Samatta. 

Kiba alisisitiza kuwa wameamua kuungana vijana kwa pamoja kwa ajili ya kufanya kitu kwenye sekta ya elimu. “Kutokana na kutambua umuhimu wa elimu nchini ndio maama tumejitolea kuwa mabalozi ambao tutahamasisha kuchangia vifaa vya kujifunzia na kufundishia na uimarishaji wa miundombinu,” alisema Alikiba. 

Nyota wa kikosi cha marafiki wa Kiba ni Shaaban Kado, Aishi Manula, Gadiel Michael, Said Ndemla, Adam Salamba, Paul Nonga, Abdul Kiba, Himid Mao, Erasto Nyoni, Agrey Morris, Ibrahim Ajib. 

Wengine ni Haruna Niyonzima, Abdi Kassim, Emmanuel Okwi, Abdi Banda, Saimon Msuva, Shaban Kisiga, Uhuru Seleman na Ramadhani Chombo. Nyota wa timu Samatta ni Juma Kaseja, Kabaly Faraji, Shomari Kapombe, Mohammedi Zimbwe, Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Athumani Chuji, Haruna Shamte, Mohammed Samatta

 Wengine ni Tresor Mputu, Thomas Ulimwengu, Farid Mussa, Haruna Moshi ‘Boban’, Amri Kiemba, Athuman Machupa, Henry Joseph, Rashid Gumbo, Mrisho Ngassa na Sultan Kaskas. 

Viingilio kwenye mchezo huo utakaochezwa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam Sh2000 kwa mzunguko huku jukwaa maalum ‘VIP’ ikiwa ni buku tatu Sh3000

No comments

Powered by Blogger.