Full-Width Version (true/false)


Angalia namna MO alivyowafanyia mastaa Simba!

 
Bilionea Mohammed Dewji 'MO' ameamua kuwabadirisha mwonekano wachezaji na benchi zima la ufundi kwa kuwang'arisha na vitu adimu sana. 

Unajua vitu gani hivyo? Sasa iko hivi kwa yule atakayefanikiwa kuingia katika Hoteli ya Kilimanjaro kushuhudia utoaji wa zawadi za MO Simba Awards wataona mabadiliko makubwa kwa wachezaji na benchi zima la ufundi Simba. 

Kwani watakuwa katika vazi jipya na adimu kwani mara nyingi huwa linavaliwa na watu maarufu yaani ni suti na ule mpango wa suruali za jinsi zilizochanwachanwa, tisheti au jezi, zitakuwa hazina nafasi kabisa mahali hapo. 

Suti hizo zimeandaliwa na kugharamiwa na tajiri huyo ambaye ni shabiki wa 'kulia' na mwanachama wa Simba, MO, na kutokana na mchakato wa hisa unaoendelea hivi sasa yuko mbioni kukabidhiwa kabisa timu hiyo aiongoze. Kabla ya timu kwenda Kenya kwenye mashindano ya SportPesa, wachezaji na benchi la ufundi walikabidhi vipimo vyao kwa ajili ya vazi hilo pamoja na viatu kwa meneja wao, Richard Robart .

No comments

Powered by Blogger.