Full-Width Version (true/false)


Askofu asema kifo cha pacha walioungana ni somo kwa Watanzania

 

Askofu Jimbo Katoliki Njombe, Alfred Maluma amesema vifo vya pacha walioungana, Maria na Consolata Mwakikuti kinapaswa kuenziwa na Watanzania kukumbushana wajibu wao kwa watu wenye ulemavu. 

"Wameacha somo hilo, tuwajali watu wenye ulemavu hilo ndilo somo walilotuachia Maria na Cobsolata," amesema Akofu Maluma leo Jumatano Juni 6, 2018 katika ibada ya kuaga miili ya pacha hao. Amesema Mungu aliwaumba pacha hao kwa mfano wa sura yake na akawapa uhai kwa kipindi walichokuwa duniani. 

Amebainisha kuwa masista wa shirika la Maria Consolata wameonyesha mfano wa kuigwa kwa kuwaleta pacha hao waliofariki dunia katika hospitali ya Mkoa wa Iringa“Ni wakati wa taasisi na mashirika mengine kuweka jitihada katika kuwajali walemavu,” amesemana kubainisha kuwa ipo jamii inayoendelea kuwatenda wenye ulemavu na kuona kama kundi lisolofaa. 

"Tuishukuru pia Serikali, imetimiza wajibu wake kwa maisha ya Maria na Consolata. Katika mema mengi tuliyojaliwa kutekeleza wajibu wetu ni kusimamua uhai wa mwingine. Serikali na wote tufanye hivi kwa nia njema,” amesema.

No comments

Powered by Blogger.