Full-Width Version (true/false)


Azam FC wazidi kuibomoa Singida United

Baada ya kumchukua aliyekuwa kocha mkuu wa Singida United Hans Van Pluijm, klabu ya Azam FC pia imemsajili mshambuliaji wa timu hiyo Tafadzwa Raphael Kutinyu na ataungana na kocha Hans ndani ya kikosi hicho. 
Singida United ambao jana wametangaza kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Mbao FC Habibu Kiyombo, wamethibitisha kuwa Kutinyu anaondoka na kuelekea Azam FC tayari kwa kuitumikia timu hiyo msimu ujao.

''Hakuna cha ziada, zaidi tu ya kujivunia kukufahamu na kufanya kazi na wewe (Tafadzwa Kutinyu), kwasababu soka ni biashara, tunakutakia kila la kheri kwenye maisha yako mapya ndani ya Azam FC'', wameandika Singida United.

Azam FC wapo kwenye maboresho ya kikosi chao ambapo tayari wameshamsajili mshambuliaji Donald Ngoma lakini pia wameondokewa na nahodha wao Himid Mao ambaye ametimkia Misri.

Singida United jana imemtangaza kocha Hemed Morocco kuwa mrithi wa kocha Hans Van Pluijm huku Mkurugenzi wa timu hiyo Festo Sanga akithibitisha kuwa wataendelea kuboresha kikosi chao kwa kufuata usharui wa mwalimu.
 

No comments

Powered by Blogger.