Full-Width Version (true/false)


Azam FC yafuta mipango yake

 Mabingwa watetezi wa Kombe la (CACAFA KAGAME CUP) Azam FC imefuta likizo kwa wachezaji wake na kuwaita kambini kuanzia Juni 15, tayari kwa kuanza maandalizi ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, inayotarajiwa kuanza Juni 28 hadi Julai 13. 

Azam FC imelazimika kufupisha muda wa mapumziko ya wachezaji wake baada ya msimu, kufuatia jana Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kutoa ratiba ya michuano ya Kagame.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga amesema wamefurahia michuano hiyo kufanyika mjini Dar es Salaam na watatumia fursa ya kucheza nyumbani kutetea Kombe lao pamoja na kocha wao mpya Hans van der Pluijm kukiandaa kikosi kwaajili ya msimu ujao.
Azam FC, itaanza kutetea ubingwa wake kwa kuvaana na Kator FC ya Sudan Kusini mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam Juni 29.

Azam FC ilitwaa ubingwa huo Agosti 2, 2015 wakati michuano hiyo ilipofanyika kwa mara ya mwisho hpaa nchini kwa kuifunga Gor Mahia mabao 2-0. Mabao hayo yalifungwa na John Bocco ambaye yupo Simba kwasasa na Kipre Tchetche anayecheza nchini Malaysia hivi sasa.

No comments

Powered by Blogger.