Full-Width Version (true/false)


Baada ya Vanessa, Diamond na Alikiba, Wakazi atunukiwa tuzo ya Nyota wa Mchezo

Rapper Wakazi ametunukiwa Tuzo maalum (Plaque) ya Nyota wa Mchezo kwa kuweza kutoa album ‘Kisimani’ na kufanya vizuri kwenye muziki kama msanii mwenye uwezo wa mkubwa wa mitindo huru, (BestFreestyler, Dopest MC, Lyricist).
Wakazi amepewa tuzo hiyo kwa kutambua mchango wake kwenye Muziki wa Hip Hop katika kipindi hiki.

Tuzo hiyo huwa zinatolewa na kituo cha radio, Times FM kupitia show ya The Playlist bila kushindanisha watu, ni tuzo maalum kwa ajili ya kutambua, kupongeza, kuwapa nguvu na kuhamasisha wasanii.

Wakazi anakuwa msanii wa nnne kupokea tuzo hiyo mara baada ya Vanessa Mdee, Diamond Platnumz na Alikiba.

Kwa upande wa Wakazi amesema kuwa kupitia ukura wake wa Instagram ameandika; Kuwa recognized kutokana na ubora wa kile ambacho unafanya especially when you spend hours day and night to get better at, is simply ecstatic. Asante sana uongozi mzima wa Times FM, and the most amazing host Lil Ommy kwa heshima hii.

No comments

Powered by Blogger.