Full-Width Version (true/false)


Babu Tale kurudisha penzi la Diamond na Zari

Miongoni mwa Mameneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale amesema kurudisha penzi la muimbaji huyo na mazazi mwenzie, Zari The Boss Lady ni kitu kirahisi.
Kauli ya Babu Tale inakuja baada ya Diamond kuachia video ya wimbo wake ‘Iyena’ na kuonekana Zari ambaye alitangaza kuachana na muimbaji huyo.

Kitendo hicho kimekuja kutonesha kidonda cha mashabiki ambao walikuwa wakifurahia couple hiyo na kutamani warudiane. Sasa Babu Tale kalisikia hilo na kuliona pia, kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;
Naona watu mnaniandikia niwarudishe Mr and Mrs dangote, ili kwangu ni kama kumsukuma mlevi yani kazi ndogo sana, ila Niliwaacha tu kwanza kila mtu sumu na hasira za mioyo yao ziwaishe ili wakirudiana akili iwakae sawa.

Sasa naona muda muafaka wa kulitumia jina langu ipaswavyo, kama ambayo mama Tee ananiita “Godfather”, siendi na magoti wala kutambaa nitapanda ndege kwenda hadi SA kuongea na mtumzima mwenzangu na ninaamini yataisha kwa asilimia 100, wananzengo niende nisiende?.
Utakumbuka February 14 siku ya wapendanao (Valentine Day) Zari The Boss Lady alitangaza kuvunja kwa mahusiano yake na Diamond kwa kile alichodai muimbaji huyo anavunja utu wake katika mitandao kwa kuwa na wanawake tofauti tofauti.

No comments

Powered by Blogger.