Full-Width Version (true/false)


Bado Siridhishwi na utendaji kazi- Rais Magufuli
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amedai kutoridhishwa na utendaji kazi wa Benki ya kilimo nchini kwa kushindwa kutimiza majukumu ya msingi ya kutoa mikopo ya kwa wakulima nchini. 

Rais Magufuli amesema hayo leo Juni 4, 2018 katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa programu ya kuendeleza Sekta ya Kilimo awamu ya pili, ameongeza kuwa licha ya Serikali kutoa pesa kwaajili ya kusaidia wakulima lakini Benki hiyo imekua ikifanya biashara na Benki nyingine

“Benki hii ipo kwaajili ya kukopesha wakulima, Serikali imekopa pesa kutoka Benki ya maendeleo Afrika ili ziende kwenye Benki hii zikakopeshe wakulima, yenyewe inazichukua inaenda kufanya biashara na Benki nyingine na ndiyo maana nasema siridhishwi na utendaji wa Benki hii, Wizara ya Fedha ipo, Mkurugenzi wa Benki na Gavana yupo lakini hakuna chochote kinachofanyika” amesema Rais Magufuli.

Rais Dkt Magufuli, ameongeza kuwa mwaka 2017 Benki hiyo ilitenga shilingi bilioni 5.2 tu kwaajili ya wakulima, lakini iliweza kukopesha Benki nyingine kiasi cha shilingi billioni 82.3 na kuwekeza katika Benki ya uwekezaji shilingi bilioni 9.2 pamoja na kununua dhamana za Serikali zenye thamani ya shilingi bilioni 3.

Mwaka 2014, Serikali ilianzisha Benki ya kilimo na kutoa kiasi cha shilingi bilioni 60 kama mtaji ikiwa na jukumu la kutoa mikopo kwa wakulima nchini na mwaka 2017 Serikali ilikopa kiasi cha shilingi bilioni 207 kutoka Benki ya Maendeleo Afrika kwa ajili ya kuongeza mtaji katika Benki hiyo.

No comments

Powered by Blogger.