Full-Width Version (true/false)


Bakwata yazifungia ’ taasisi nne kusafirisha mahujaji


 
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limewatoa hofu waislamu wanaotarajia kwenda kwenye ibada ya hijja, likieleza kuwa limejipanga vyema kuhakikisha upungufu uliojitokeza mwaka jana haujirudii. 

“Taasisi nne ambazo ni Tanzania Chartable Oraganization, Haji Khikma, Taquwa Haji Group na Almadina Social Services Trust hazitosafirisha mahujaji kwa kuwa hazijakidhi masharti yaliyowekwa. Hatutaki mambo yaliyojitokeza mwaka jana, yajirudie sasa,” amesema Sheikh Hamisi Mataka, mwenyekiti wa baraza hilo. 

Mataka ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Juni 2, 2018 jijini hapa, katika mkutano wake na waandishi wa habari, kubainisha kuwa zaidi ya mahujaji 100 mwaka, 2017 walikwama kwenda kufanya ibada hiyo baada ya taasisi ya Twaiba iliyokusanya fedha zao kwa madai ya kuwawezesha kusafiri, kuingia mitini. 

“Mpaka sasa mambo yote yanakwenda vizuri, hakuna tishio lolote ambalo tumelibani la mahujaji kutosafiri kwa sababu mambo yote yapo katika mstari kuhakikisha kuwa waislamu wanatekeleza ibada hiyo,”amesema Mataka.Mataka alisema taasisi 11 pekee ndizo zilizokidhi vigezo na msharti yaliyowekwa ikiwemo , Alhusna Haji Trust, Shamsul Maarifa Kheri na Tanzania Muslim Development Asociatiaon, Tanzania Muslim Haji Trust. 

Katika hatua nyingine Mataka amessema kuanzia Juni 8, 2018 waislamu nchini kupitia misikiti yao watafanya harambee ya kuchangia maendeleo ya baraza hilo ili liweze kutekeleza majukumu yake mbalimbali, ikiwemo kuwalipa watumishi.

No comments

Powered by Blogger.