Full-Width Version (true/false)


Balaa lingine tena, Simba na Yanga zapangwa kundi moja Kagame CupMahasimu wa soka nchini Simba na Yanga, wanatarajia kukutana tena kwenye michuano ya Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu kama (CECAFA KAGAME CUP), baada ya kupangwa kundi moja kwenye michuano ya mwaka huu. 

Akiongea leo jijini Dar es salaam mbele ya waandishi wa habari, Katibu mkuu wa CECAFA Nicholaus Msonye, amesema michuano hiyo msimu huu itakuwa na makundi matatu ambapo bingwa wa Tanzania Simba atakuwa kundi C pamoja na hasimu wake Yanga.

Michuano hiyo itashirikisha jumla ya timu 12, zikiwemo timu tatu kutoka Tanzania Bara ambazo ni Simba, Yanga na bingwa mtetezi wa Kombe hilo Azam FC pamoja na JKU kutoka Zanzibar hivyo kukamilisha timu 4 zinazotoka Tanzania.

Mashindano ya mwaka huu yanaanza tarehe 28 Juni, 2018 na kumalizika tarehe 13 Julai 2018. Yatafanyika kwenye viwanja viwili ambavyo ni Uwanja wa Tiifa jijini Dar es salaam pamoja na Chamazi Complex.

Kundi A:
Azam FC (Tanzania Bara)
JKU (Zanzibar)
Kator FC (Uganda)
Polisi Uganda FC (Uganda). 


Kundi B:
Rayon Sports (Rwanda),
Gor Mahia (Kenya),
AS Port (Djiboud)
Lydia LB Academy (Burundi). 


Kundi C:
Yanga SC (Tanzania Bara),
Simba SC (Tanzania Bara),
St. George (Ethiopia)
Dekadaha FC (Somalia). 

No comments

Powered by Blogger.