Full-Width Version (true/false)


Bayern yampiga bei Vidal


 
Bayern Munich imeamua kuweka sokoni masupastaa wake, lakini piga kwa timu zilizoshindwa kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, zisijimbue kabisa kupeleka ofa zao za kuwataka mastaa hao. 

Mastaa ambao Bayern Munich ameamua kuwapiga bei ni Arturo Vidal, Thiago Alcantara, Jerome Boateng na Julian Bernat, lakini staa wa kimataifa wa Chile, Vidal amesema hawezi kukubali tu ofa na atakubali kujiunga na timu nyingine itakayokuja kumfuata kama tu itacheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. 

Jambo hilo ni sawa pia kwa Thiago Alcantara, ambaye amekuwa akiwindwa Manchester United kwa muda mrefu pamoja na Boateng, ambaye hakika hatahitaji kwenda kucheza timu ambayo haitampa nafasi ya kucheza soka la Ulaya msimu ujao. 

Bayern Munich inataka kusafisha kabla ya kocha mpya Niko Kovac, anayekuja kuchukua mikoba ya Jupp Heynckes hajaanza kufanya kazi yake. 

Kuna uwezekano wa mastaa hao wakaenda kuungana na kocha wao wa zamani Carlo Ancelotti huko Napoli, kwa sababu ni timu ambayo inawapa nafasi ya kucheza kwenye michuano ya Ulaya msimu ujao.

No comments

Powered by Blogger.