Full-Width Version (true/false)


Bodi ya Utalii imeamua kutangaza vivutio vyake kwa kuwatumia viziwi.

 

Bodi ya Utalii Tanzania TTB, imeendelea kutangaza vivutio vyake vya utalii wa ndani kwa kuwahusisha walemavu viziwi zaidi ya 60 wa mkoa wa Mwanza kwa kutambua mchango wao katika kukuza, kuimarisha na kuendeleza sekta hiyo. 

Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania Geofrey Meena amesema lengo kubwa la kutoa elimu hiyo kwa walemavu viziwi ni kuwawezesha kujua vivutio muhimu vilivyopo nchini ili wapate fursa ya kuvipenda, kuvitembelea na kuvitangaza nje ya nchi kupitia vyama vyao raki. 

Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Maendeleo ya viziwi Tanzania ( TAMAVITA ) Kelvin Nyema,kupitia kwa Mkalimani wa lugha ya alama mkoa wa Mwanza Subira Joseph, amesema kukua kwa sekta ya utalii nchini kunatokana na utendaji mzuri wa bodi hiyo na kutokuwepo kwa upendeleo wa aina yoyote. 

Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya miundombinu mkoani Mwanza Seif Hussein, amesema elimu hiyo itawapa mwangaza walemavu viziwi kujua haki zao katika uhifadhi wa mazingira na kuzuia ujangiri dhidi ya wanyamapori katika hifadhi za taifa.

No comments

Powered by Blogger.