Full-Width Version (true/false)


Buffon afungiwa na UEFA

Chama cha soka Ulaya UEFA leo kimetangaza kufikia maamuzi ya kumfungia golikipa wa club ya Juventus ya Italia Gianluigi Buffon baada ya kujiridhisha kuwa alionesha utovu wa nidhamu.


UEFA wamefikia maamuzi ya kumfungia mechi tatu Buffon baada ya kujiridhisha kuwa, golikipa huyo alitenda kosa wakati wa mchezo wa UEFA Champions League kati ya Juventus dhidi ya Real Madrid kwa kumtolea refa Michale Oliver maneno yasiofaa.


Buffon kapewa adhabu hiyo kutokana na kuoneshwa kadi nyekundu dakika ya 93 ya mchezo wakati akipingana na refa Oliver kuhusu maamuzi yake ya kuamuru penati ipigwe dhidi ya timu yake ya Juventus.

No comments

Powered by Blogger.