Full-Width Version (true/false)


Bunge latoa rambirambi kifo cha Maria na Consolata

  

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema Bunge limepokea kwa masikitiko makubwa vifo vya pacha Maria na Consolata. 

Akitoa salamu hizo za rambirambi leo bungeni Juni 4, 2018, Spika Ndugai amemwomba Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako kufikisha salamu kwa ndugu, jamaa na marafiki. 

Huku ukumbi wa Bunge ukiwa kimya kumsikiliza akitoa salamu hizo, Spika Ndugai amesema: 

“Kwa niaba ya Bunge nitoe salamu za rambirambi kifo cha Maria na Consolata.” “Walikuwa ni watoto wa ajabu na wenye upendo. Kifo chao kimetupa masikitiko makubwa sana. Waziri wa Elimu (Profesa Ndalichako) tufikishie salamu huko,” ameongeza.

No comments

Powered by Blogger.