Full-Width Version (true/false)


Bwawa la Nyumba ya Mungu Lafurika Maji Tena....Watu 300 Hawana Pakuishi Baada ya Kuzingiwa Maji


Wakazi zaidi ya 300 wa kijiji cha Ruvu Jitengeni wilayani Same mkoani Kilimanjaro hawana makazi ya kuishi baada ya nyumba zao kujaa maji kutokana na bwawa la Nyumba ya Mungu kujaa maji kupita kiasi.

Mkuu wa wilaya ya Same, Rosemary Senyamule amesema kitongoji cha Mvungwe ndicho kimeathirika zaidi na mafuriko, tayari Serikali imeanza jitihada za kuwahamisha wakazi wake.

Kijiji cha Ruvu Jitengeni kitakuwa cha tatu kukumbwa na mafuriko tangu Mei 19, 2018 yaliyoacha zaidi ya watu 2,500 bila makazi kutokana na bwawa la Nyumba la Mungu kujaa maji kupita kiasi.

No comments

Powered by Blogger.