CCM yaihakikishia jumuia ya kimataifa mazingira wezeshi na rafiki ya uwekezeshaji nchini
Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kimeihakikishia Jumuia ya kimataifa mazingira
mazuri, wezeshi na rafiki kwa uwekezaji nchini. Kauli ya CCM imetolewa
leo na Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.
Akiambatana
na Maafisa wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) Ndg.
Polepole amefanya mazungunzo ya kirafiki na Mabalozi wawili Bi. Matli na
Bwana Arthur Matli wa nchi ya Uswisi wanaowakilisha Tanzania pamoja na
Afrika Mashariki na Zambia.
Katika
mazungumzo hayo Ndg. Polepole amefafanua juu ya Mageuzi makubwa ambayo
CCM inayafanya katika Chama na Serikali na ambayo yanalenga kuongeza
tija, ufanisi na utumishi wa watu. Aidha amewajulisha Mabalozi hao kuwa
Chama kimeielekeza Serikali kupitia mikataba ya Madini ili kuhakikisha
haki ya Tanzania inapatikana na kwamba baada ya mapitio kumefanyika
majadiliano na mashauriano na wawekezaji ambao wameridhia kwa moyo mmoja
kuingia katika utaratibu mpya ambao unalinda haki ya watanzania na
wawekezaji pia.
"Chama
Cha Mapinduzi kimeendelea kuielekeza Serikali kuendelea kuweka
mazingira rafiki, wezeshi na mazuri kwa wawekezaji ambao wako tayari
kuja kuwekeza hapa Tanzania na hasa katika eneo la viwanda. Serikali
imetenga ardhi ya kutosha kwa uwekezaji mkubwa, imeweka utaratibu mzuri
kupitia kituo cha uwekezaji (TIC) na hivyo yeyote mwenye nia ya kuwekeza
anakaribishwa. Kama kuna mwekezaji ambaye amepata changamoto katika
mchakato wa kuwekeza nchini au anapata ugumu wowote asisite kutoa
taarifa na Serikali ya CCM itashughulikia changamoto hizo" amesema Ndg.
Polepole.
Naye
Balozi wa Uswisi nchini Tanzania amesema amefarijika sana kwa
mazungumzo na yamemwongezea Imani zaidi kwasababu amepata kujua mambo
mengi tofauti na habari ambazo anazisikia zikiwemo zinazopotoshwa. "Nakuhakikishia
kwamba wakati wowote atakapopatikana mwekezaji nitamleta mara moja
Tanzania, na ninapendekeza utaratibu huu wa mazungumzo uendelee" amesema
Bi. Matli Balozi wa Uswisi Nchini Tanzania
Huu ni mwendelezo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuimarisha mahusiano ya ndani na nje katika eneo la siasa, diplomasia na uchumi.
Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
OND LUMUMBA
No comments