Full-Width Version (true/false)


CHADEMA kukata rufaa
Wakili wa utetezi katika kesi Na. 112/2018 inayowakabili Viongozi Wakuu wa CHADEMA wakiongozwa na M/kiti Mhe Freeman Mbowetz na Wabunge kadhaa wa chama hicho, Peter Kibatala ameieleza mahakama kusudio la kukata rufaa kutokana na kutoridhishwa na uamuzi wa mahakama. 
Kibatala ametoa taarifa hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya hakimu huyo kuamuru upande wa mashtaka kufanya mabadiliko katika hati ya mashtaka.

Mawakili upande wa utetezi wakiongozwa na Kibatala na Jeremiah Mtobesya walikuwa wakiomba mashtaka yanayowakabili washtakiwa hao yafutwe kwa sababu yana upungufu wa kisheria, ikiwamo shtaka moja kuwa na makosa mawili hoja ambayo ilipingwa na upande wa mashtaka. 

Hata hivyo, baada ya Hakimu Mashauri kupitia hoja za upande wa utetezi ameamurukufanyike upande wa mashtaka kufanya marekebisho katika hati ya mashtaka yanayomkabili Mwenyekiti huyo pamoja na viongozi wengine wa chama hicho.

Baada ya kutoa uamuzi huo, Wakili Kibatala aliieleza mahakama kuwa hawajaridhishwa na uamuzi huo hivyo aliwasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 12 ikiwamo kula njama, kufanya mkusanyiko usio halali kinyume cha sheria na kuendelea kufanya mikusanyiko usio halali ama maandamano yaliyosababisha kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.

Mbali na Mbowe wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, Naibu Makatibu wakuu Salum Mwalimu (Zanzibar) na John Mnyika (Bara) Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Mbunge wa Bunda Ester Bulaya.

Kesi hiyo Na. 112/2018  imehairishwa mpaka kesho Jumanne 12/6/2018 kwa ajili ya mahakama kutoa maamuzi.

No comments

Powered by Blogger.