Full-Width Version (true/false)


Chanzo cha ajali treni na basi chaanikwa

Ikiwa yamepita masaa kadhaa tokea ilipotokea ajali ya basi la abiria kampuni ya Prince Hamida kugongana na treni ya mizigo Mjini Kigoma, Jeshi la Polisi limebaini chanzo cha ajali hiyo kuwa kimesababishwa na uzembe wa dereva wa basi hilo kwa kushindwa kuchukua tahadhari. 
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma Martin Otieno, wakati alivyokuwa akifanya mahojiano maalum ndani ya kipindi cha East Africa Drive kilichorushwa alasiri ya leo Juni 06, 2018 kutoka East Africa Radio na kusema mpaka sasa hivi watu 10 wameshafariki kutokana na ajali hiyo.

"Mpaka sasa hivi wameshafiriki jumla ya watu 10 na saba walifariki pale pale enoo la tukio lakini wengine watatu walifariki wakati wanakimbizwa kupelekwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu. 

Jumla ya majeruhi waliokuwa 27 waliokuwa wanatibiwa lakini kati ya hao wanne tayari wamesharuhusiwa kurudi majumbani mwao", amesema Kamanda Otieno

Pamoja na hayo, Kamanda Otieno ameendelea kwa kusema "hali zao kwa sasa hivi zinaendelea vizuri labda kama itakuja kubadilika kwa hapo baadae lakini chanzo cha ajali hiyo kimetokana na uzembe wa dereva wa gari wa kutochukua tahadhari wakati anapita katika eneo la reli".

No comments

Powered by Blogger.