Full-Width Version (true/false)


Chelsea yapigwa bei

 

Habari ndiyo hiyo mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich ni kama vile ameiweka sokoni klabu hiyo yenye maskani yake Stamford Bridge. 

Ripoti zinadai kwamba bilionea Abrahimovich hataweka ngumu kama kutawekwa mezani Pauni 1 bilioni kwa ajili ya kuipiga bei Chelsea, hiyo ina maana kwamba ndicho kiwango kinachopaswa kuuzwa kwa kikosi hicho cha London. 

Taarifa zinadai kwamba bilionea huyo wa Russia atahitaji kiasi cha Pauni 1.17 bilioni kama atafikia uamuzi wa kuipiga bei timu hiyo anayomiliki hasa baada ya sasa kuingia kwenye utata mkubwa wa kushindwa kupata kibali cha kwenda kuishia Uingereza. 

Abramovich kwa sasa hayupo England na mambo yamezidi kuvurugika zaidi kwenye kikosi hicho cha Chelsea baada ya kuahirisha mpango wao wa kuongeza uwanja wa Stamford Bridge utakaohitaji Pauni 1 bilioni kutokana na tatizo la uchumi. 

Tajiri kwa sasa anaonekana kwamba hayupo tayari kufanya uwekezaji mkubwa kwenye nchi ambayo serikali yake haitaki kumpa kibali cha kuishi. Bilionea huyo ameshawekeza zaidi ya Pauni 1 bilioni tangu alipoinunua timu hiyo Juni 2003 kwa Pauni 140 milioni. 

Kwa mujibu wa Forbes, Chelsea ni klabu namba saba yenye thamani zaidi duniani ikitajwa kuwa na thamani ya Pauni 1.44 bilioni

No comments

Powered by Blogger.