Full-Width Version (true/false)


China yasema matamshi ya Marekani ni ya 'kijinga'


 
China imetaja kuwa matamshi ya 'kijinga' yanayotolewa na Marekani kwamba inawatishia na kuwashurutisha majirani zake kupitia kupeleka silaha katika bahari ya kusini mwa China

Jenerali wa ngazi ya juu nchini China alisema kuwa China ina haki ya kupeleka majeshi na silaha katika himaya yake.

Awali waziri wa Ulinzi nchini Marekani James Mattis alisema kuwa vitendo vya Beijing vilizua maswali mengi kuhusu malengo yake.

Mataifa sita yanapigania visiwa hivyo , lakini China imepiga jeki madai yake kwa kujenga katika visiwa hivyo mbali na kupiga doria.

Jenerali Mattis alitoa matamshi hayo katika mkutano wa usalama nchini Singapore.

Akizungumza katika mkutano huohuo Luteni jenerali wa China He Lei alisema: Matamshi yoyote ya 'kijinga' kutoka mataifa mengine hayawezi kukubalika.

Jenerali He alisema hatua ya Bejing kupeleka wanajeshi wake ni kutokana na sera yake ya kujilinda , akiongezea kuwa lengo lao kuu ni kuzuia uvamizi wowote

''Ukiwa katika himaya yako unaweza kupeleka majeshi na silaha''.
Aliongezea: Tunachukulia taifa lolote linalojaribu kupiga makelele kuhusu hatua hii kama taifa linalojaribu kuingilia maswala yetu ya ndani.

Jenerali Mattis alisema kuwa China ilipekeka zana za kijeshi na makombora ya kudungua ndege katika maeneo ya visiwa hivyo vilivyopo kusini mwa bahari ya China. 

Alisema kuwa lengo la China kupeleka vifaa hivyo na wanajeshi ni kuwatishia na kuwashurutisha majirani zake

No comments

Powered by Blogger.