Full-Width Version (true/false)


Cristiano Ronaldo awashtua mashabiki wa Real MadridMchezaji bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo amewashtua mashabiki wa klabu ya Real Madrid baada ya kuzagaa taarifa kuwa aliwatangazia wachezaji wenzake wiki moja kabla ya kuivaa Liverpool mchezao wa fainali wa klabu bingwa barani Ulaya kuwa na mpango wa kuondoka Bernabeu.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 33, huwenda akaondoka Bernabeu msimu huu baada ya kuisaidia Real kutwaa taji la klabu bingwa barani Ulaya kwa ushindi wa jumla ya mabao 3 – 1 dhidi ya Liverpool huko Kiev.


Kupitia mahojiano yake na chombo cha habari cha beIN Sports, Ronaldo amesikika akisema kuwa anajiskia furaha ya kuwa Real licha ya siku chache zijazo akitarajia kutoa hatima yake kwa mashabiki.
”Najiskia furaha kuwa Real Madrid, siku chache zijazo nitawapatia majibu mashabiki ambao siku zote wamekuwa upande wangu,’amesema Ronaldo.


Inasadikika kuwa mshindi huyo mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or anatishia kuondoka Real ili kupata mkataba mpya utakao mfanya kuingiza kitita kikubwa cha fedha hii ikiwa ni baada ya kuona mpinzani wake, Lionel Messi kuwa mchezaji wa kwanza anaevuta mkwanja mrefu baada ya kuingia dili hilo mwanzoni mwa msimu na timu yake ya Barcelona na kukusanya pauni milioni 35 kwa msimu

No comments

Powered by Blogger.