Daktari matatani kwa kuuza dawa zilizo 'expire''
MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Nyanda
za Juu Kusini, imemnasa daktari wa Hospitali ya Wilaya ya
Mbozi mkoani Songwe, Godfrey Pakrasi, kwa tuhuma za
kuuza dawa zilizokwisha muda wake katika duka lake la
dawa.
Kadhalika, daktari huyo anatuhumiwa kukutwa akiuza dawa za serikali zenye nembo ya Bohari Kuu
ya Dawa (MSD).Daktari huyo alikamatwa jana wakati maofisa hao wakifanya operesheni ya
kushtukiza mkoani Songwe.
Kwa upande wake Dk. Pakrasi alikiri kukutwa na dawa hizo sambamba na kutibu kisukari na moyo
akitumia kifaa cha serikali huku akielezakuwa alikuwa kwenye harakati ya kuziondoa dawa hizo
kwani duka hili amelinunua kwa mtu na pia baadhi ya dawa amekuwa kizinunuamitaani.
Silvester Mwidunda, Ofisa Mkaguzi wa TFDA, alisema waliamua kufanya upekuzi wa kushtukiza
baada ya kubaini uwapo wa baadhi yawafanyabiashara wasio waaminifu ambao wamekuwa wakitoa
tiba kwa dawa bandia na zilizokwisha muda wake.
Alisema duka la daktari huyo lilikutwa na makosa mengi, lakini pia halijasajiliwa huku yeye akiwa
hana sifa ya kuendesha duka hilo kwa kuwa hajapata mafunzo ya ARDO, na kuwa TFDA inalifunga
hadi atakapofanikiwa kukamirisha taratibu zote.Kutokana na hali hiyo, ofisa huyo aliamuru daktari
huyo akamatwe ambapo Jeshi la Polisi lilimkamata na kwenda naye kumhoji, lakini aliachiwa
baadaye kwa dhamana.
Diwani wa kata hiyo, Kennan Mbughi, alisema akiwa mjumbe wa Kamati ya Afya katika
halmashauri hiyo atalipeleka suala hilo kwenye vikao, ili mamlaka husika ifanye kazi ya ukaguzi
mara kwa mara katika maduka ya dawa ili kuokoa maisha ya watu.
No comments