Dk. Shika amtambulisha msanii wake, adai atafunika wasanii wengi
Dk. Shika leo, Juni 8, 2018 katika Mkutano wake na Waandishi wa
habari amemtambulisha Msanii wake mpya atakaye kuwa anamsimamia katika
zake za muziki aitwaye Godson ambaye pia ametambulisha nyimbo yake mpya
iitwayo ‘Relux’.
Dk. Shika katika Mkutano wake huo amesema kwa msanii yoyote
atakayetaka kusimamiwa na yeye yupo tayari lakini anaanza na huyo
aliyemtambulisha kwa siku ya leo.
“Nina uhakika kwamba atafunika wasanii wengi , kwahiyo jaribuni kumfuatilia,” amesema Dk. Shika.
Dk. Shika ni daktari wa magonjwa ya binadamu, aliyejipatia umaarufu
miezi kadhaa iliyopita kupitia kufika dau wakati wa mnada wa Majumba ya
Lugumi.
No comments