Full-Width Version (true/false)


Dodoma:Mwalimu mkuu mbaroni kwa kumbaka mwanafunzi wake.

 


Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia Bwana Shaidu Twahil ambaye ni mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Hijira  iliyopo jijini Dodoma kwa tuhuma za  kumbaka mwanafunzi wake wa kidato cha nne mwenye umri wa miaka 17. 

Akizungumza kwa njia ya simu na ITV Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa polisi Gilles Muroto amesema Jeshi la polisi limetia mbaroni mtuhumiwa ambapo anataraji kukishwa mahakamani na kudai kuwa hatua za kisheria zitachukua mkondo wake. 

ITV imezungumza na mwanafunzi huyo ambaye amekiri kurubuniwa na mwalimu ambapo amesema ameathirika kisaikolojia na kushindwa kuendelea na masomo yake huku akiiomba serikali kuongeza nguvu katika udhibiti wa vitendo vya ubakaji ambavyo vimekuwa vikiongezeka. 

Kwa upande wake mama mzazi wa mwanafunzi huyo  amesema kitendo hicho si cha kuvumilia na kwamba mtoto wake amelazimika kuacha masomo na kuiomba serikali iingilie kati ili mwanae aweze kuendelea na masomo huku mmoja wa wakazi wa mkoa wa Dodoma akisema  vitendo vya namna hiyo vinazidi kushamiri na kuhatarisha usalama wa watoto .

 credit:ITV

No comments

Powered by Blogger.