Full-Width Version (true/false)


Donald Ngoma Kurejea Leo Akitokea Afrika Kusini kwa Matibabu

 

Mshambuliaji mpya wa Azam FC, Donald Ngoma, anawasili leo nchini akitokea Afrika Kusini alipokuwa amepelekwa kufanyiwa vipimo vya afya.
Ngoma alikuwa katika jiji la Cape Town kwa ajili ya vipimo hivyo ambavyo tayari vimekamilika na leo mchana Daktari wake atatoa ripoti ya matokeo ya vipimo hivyo.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa klabu ya Azam, Jaffer Idd, amesema Ngoma atawasili majira ya leo mchana akiwa sambamba na daktrari wake aliyeenda naye Afrika Kusini.

Ikimbukwe Ngoma alishindwa kucheza talribani mechi zote za msimu uliopita kutokana na kusumbuliwa na majeraha wakati akiwa Yanga.

Mapema baada ya kuingia naye mkataba, Azam waliazimia kumsafirisha mpaka Cape Town kwa ajili ya kufanyiwa vipimo kiafya.

No comments

Powered by Blogger.