Full-Width Version (true/false)


Fainali ni Simba na Gor Mahia ,hapatoshi Nakuru

 


Yametimia bingwa wa Tanzania Bara, Simba na bingwa wa Kenya, Gor Mahia zitakutaka kwa mara ya kwanza katika fainali ya mashindano ya Sportpesa Supercups. 

Mabingwa watetezi Gor Mahia imefuzu kwa fainali baada ya kuichapa Singida United kwa mabao 2-0 katika mchezo mkali uliotibuliwa mvua iliyosababisha wachezaji kuteleza hovyo. 

Mshambuliaji mkongwe Gor Mahia, Meddi Kagere alifunga mabao yake mawili kila kipindi bao moja na kuhakikishia miamba hiyo ya Kenya kutinga fainali na rekodi ya kufunga mabao 5 katika mechi mbili. 

Fainali itawakutanisha Gor Mahia na Simba iliyotinga hatua hiyo baada ya kuitoa Kakamega Homeboyz kwa penalty 5-4 katika nusu fainali ya kwanza. 

Mshindi wa fainali hiyo atapeta fedha pamoja na tiketi ya kwenda England kucheza mechi dhidi ya Everton kwenye Uwanja wa Goodison Park, Liverpool. Singida United na Homeboyz zenyewe zitaonyeshana kazi katika kuwania mshindi wa tatu wa mashindano hayo.

 Yanga pamoja na kutolewa mapema imekuwa timu pekee ya Tanzania ambayo imefanikiwa kufunga bao ndani ya dakika 90 za mashindano hayo hadi sasa hatua ya nusu fainali.

No comments

Powered by Blogger.