Full-Width Version (true/false)


Familia ya Diamond yamwangukia Zari

 
 
Habari iliyobamba katika mitandao leo ni kuhusu video ya wimbo mpya wa Diamond Platnumz, Iyena, ambayo imeachiwa saa 16 zilizopita. 
 
Kutoka kwa wimbo huo kumesababisha familia ya staa huyo kutumia fursa ya kumuangukia aliyekuwa mpenzi wake, Zari Hassan na kuzua mjadala katika mitandao. 
 
Katika mtandao wa Instagram, mama mzazi wa mwanamuziki huyo, Sanura amekuwa akiweka picha akiambatanisha na maneno ya kumsifu mwanamke huyo anayeishi nchini Afrika Kusini. 
 
Mwingine kutoka familia ya Diamond aliyeshiriki katika mjadala huo ni dada yake, Esma ambaye amemsifu wifi yake huyo wa zamani kwa usafi. 
 
Wapo ambo wanaojiita timu Hamisa waliomtetea mwanamitindo huyo wakimtaka Diamond arekodi upya video hiyo kwa kuwa hiyo imefanyika Septemba mwaka jana kabla ya Zari kutoa tamko la kuachana na mzazi mwenzake huyo.

No comments

Powered by Blogger.