Full-Width Version (true/false)


Gormahia bingwa Sportpesa super cup, yaitoboa Simba 2-0
Klabu ya Gormahia ya nchini  Kenya imefanikiwa kuchukua ubingwa wa michuano ya Sportpesa kwa kuifunga klabu ya Simba ya Tanzania goli 2-0.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Afraha mjini Nakuru, Gor Mahia walitawala zaidi mchezo wakiwa na kikosi chao kamili huku Simba wakipata wakati mgumu kutengeneza nafasi za kufunga.
Gor Mahia wamejipatia mabao yao kupitia kwa Mshambuliaji wao hatari, Medy Kagere aliyefunga la kwanza katika dakika ya 6 tu ya mchezo na kufanya kipindi cha kwanza kiende kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili kilianza tena kwa Gor Mahia kuzidi kulisakama lango la Simba wakionesha njaa ya kupata goli jingine ambapo mnamo dakika ya 54, Tuyisenga alifunga bao la pili kwa kumalizia mpira wa krosi uliopigwa kutoka kulia mwa Uwanja na kumuacha Kipa Aishi Manula akiwa hana cha kufanya.Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Gormahia kuchukua ubingwa huo baada ya mwaka jana kuchukua ubingwa huo ambao mashindano yake yalifanyika nchini Tanzania.Gormahia wamejikatia tiketi ya kwenda Goodison Park nchini uingereza kucheza dhidi ya Everton.

No comments

Powered by Blogger.