Full-Width Version (true/false)


Halima Mdee: Naona aibu Wazir Kabudi kuwa mwalimu wangu kwa anayoyafanya

 


Mbunge wa Kawe (Chadema) Halima Mdee amesema anaona aibu kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi kuwa mwalimu wake kwa sababu ameshindwa kulieleza Bunge kuhusu Sh424 trilioni ambazo Serikali ilidai zitalipwa na Mgodi wa Acacia kama kodi waliyokwepa. 

Akichangia bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa fedha 2018/19, Mdee amesema wakati Profesa Kabudi akizungumza bungeni alisema hawatasema tena kiasi wanachodai kwa makampuni hayo kwa sababu kuna watu wanaibuka kuidai nchi. 

“Tuliwahi kusema kuwa shida si Acacia, shida ni Serikali. Naona aibu kusema kuwa Kabudi ni mwalimu wangu, waziri anasema kuwa hawezi kutamka kiasi gani kimelipwa kwasababu watakuja watu wanaotudai,’’amesema.

 Hata hivyo, alikatizwa na maombi ya taarifa kutoka kwa wabunge wa CCM na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu) na hivyo muda wake wa kuchangia kuisha

No comments

Powered by Blogger.