Full-Width Version (true/false)


Harmonize kuwapandisha jukwaa moja Sara na Wolper

 


Mwanamuziki Harmonize anatarajiwa kuwakutanisha wapenzi wake Jackline Wolper na Sara katika jukwaa moja katika tamasha lake la Usiku wa Kusi. 

Wolper na Sara wamekuwa katika vita ya maneno ya kila mmoja kujaribu kuhakikisha ndiye anakuwa karibu zaidi na Harmonize. 

Harmonize jina lake halisi ni Rajabu Abdul alisema wawili hao atawakutaniaha Sikukuu ya Idd ya pili viwanja vya Dar Live katika tamasha lake la Usiku wa Kusi. 

Alisema katika shughuli yote hiyo, Wolper atakuwa anaisimamia ikiwemo kuwaita wasanii wa kupanda jukwaani. 

"Lengo la kumualika Wolper ni katika kufuta tofauti zetu mbele ya mashabiki kwani naamini Wolper ana mashabiki wengi na mimi vilevile hivyo isije ikafika mahali tukawagawa kwa ajili tu tuna uhasama. Mbali na kuwepo kwa wasanii wa bongofleva, Harmonize alisema usiku huo kutakuwa na ngoma za kutoka mikoa ya kusini

No comments

Powered by Blogger.