Full-Width Version (true/false)


Hatimaye kocha wa Simba ameonekana jukwaani

 


Nakuru. Baada ya sintofahamu ya alipo kocha wa Simba, Mfaransa, Pierre Lechantre aliibukia jukwaani wakati mabingwa hao wakicheza nusu fainali ya Kombe la Mashindano ya SportPesa Super Cup dhidi ya Kakamega Homeboys. 

Akizungumzia uamuzi wa kutoka benchi leo Lechantre alisema lengo lake ni kutoa nafasi kwa msaidizi wake Masoud Djuma kuonyesha uwezo wake. 

Inasemekana kwamba Lechantre amekasirishwa na kitendo cha mabosi wa timu hiyo kumchunia kumpa mkataba mpya huku kukiwa na ukosoaji mkubwa wa namna timu ya Simba inavyocheza kwa sasa hivyo kuamua kuondoka. Lechantre alisema watazungumza kuona wanafikia wapi kuhusu hatma yake ndani ya klabu hiyo. 

Viongozi wa Simba wakiongozwa na Makamu wa Rais wa Simba, Salim Abdallah wameshindwa kuwa na majibu wa uhakika juu ya Lechantre huku wakidai kuwa watatoa taarifa kamili mara baada ya mechi hiyo ya nusu fainali. Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Said Tulily ambaye yuko na timu hiyo mjini hapa alisema watatoa taarifa kamili baada ya mchezo huo wa nusu fainali.

Lechantre alijiunga na Simba mapema mwaka huu na kufanikiwa kuipa taji la Ligi Kuu Bara walilokuwa wamelikosa kwa misimu mitano mfululizo

No comments

Powered by Blogger.