Full-Width Version (true/false)


Hazard, Mo Salah lao moja

 

England. Mshambuliaji wa Chelsea, Eden Hazard amesema haoni kitu kitakachomzuia Mohamed Salah asiende kuziteka fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza Alhamisi ijayo huko Russia. Hazard amekubali moto wa staa huyo wa Liverpool aliouonyesha msimu uliomalizika hivi karibuni na kwamba hatapunguza makali yake wakati atakapokuwa na kikosi cha Misri kwenye fainali hizo za Russia. 

Salah hakuwapo katika mechi ambayo Misri ilichapwa 3-0 na Ubelgiji ya Hazard kutokana na sasa kuuguza maumivu ya bega aliyopata katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid mwezi uliopita. "Misri ina wachezaji wazuri sana," alisema Hazard na kuongeza. “Tulichokifanya ni kumiliki mpira na kufunga mabao mapema jambo lililotufanya tuone tumepata urahisi mchezoni. 

Tumefurahi kuwafunga Misri3-0. Namtakia kila lenye heri Salah na naamini atarudi uwanjani haraka. Nitaishangilia Misri kwenye Kombe la Dunia kwa ajili yake. 

"Misri inaonekana kuwa tofauti bila ya Salah, lakini bado wanaonekana kucheza vizuri. Staili yao ya uchezaji inafanana sana na Tunisia. Nilizungumza na Salah baada ya fainali ya Ligi ya Mabinngwa Ulaya na nilimtumia meseji, ni rafiki yangu na nitapenda kumwona kwenye Kombe la Dunia."

No comments

Powered by Blogger.