Full-Width Version (true/false)


Himid Mao aiomba msamaha Azam FC
Aliyekuwa nahodha wa klabu ya soka ya Azam FC, Himid Mao ameiaga klabu hiyo rasmi baada ya kusaini kuichezea timu ya Petrojet ya Misri huku akiiomba msamaha timu hiyo na zaidi kueleza namna timu hiyo ilivyompokea akiwa kijana mdogo hadi leo amekuwa mtu mzima. 

''Nimeishi kama mwana familia kwa miaka yote nilikuja nikiwa kijana mdogo kabisa wa kidato cha kwanza naondoka nikiwa nimepevuka kimwili na kiakili, mimi ni binadamu kama kuna sehemu niliwakosea naombeni mnisamehe na mimi nimesamehe kama mlinikosea'', ameandika.

Aidha Himid pia amewashukuru viongozi wa timu hiyo kwa kuwa imara katika nyakati zote walipokuwa wanafanya vizuri na hata walipofanya vibaya waliwapa moyo na kuwajenga ili wafanye vizuri.

Licha ya viongozi wa wana lambalamba kutaka kumbakiza lakini Himid ameeleza aliwaomba akatafute changamoto mpya hivyo ilibidi wamkubalie ombi lake na tayari viongozi wamethibitisha kumaliza naye kwa amani huku wakimtakia kila la kheri.

Himid Mao amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuichezea timu ya wauza mafuta wa Misri Petrojet ambao wamemaliza ligi wakiwa katika nafasi ya 12 msimu huu. Himid ameondoka akiwa ameisaidia Azam FC kumaliza katika nafasi ya pili kwenye VPL.

No comments

Powered by Blogger.