Full-Width Version (true/false)


Huyu ndio nahodha mpya wa Brazil

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil, Gabriel Jesus ameteuliwa na kocha wa timu hiyo Leonardo Bacchi 'Tite', kuwa nahodha kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Croatia leo usiku. 

Tite amekuwa na utaratibu wa kubadilisha manahodha tangu aanze kuifundisha timu hiyo mwaka 2016, ambapo mara hii amemkabidhi kinda huyo wa miaka 21. Jesus mwenyewe amesema yupo tayari na atajitahidi kukitendea haki kitambaa hicho.

Mchezo huo wa kirafiki utapigwa nchini England kwenye uwanja wa klabu ya Liverpool (Anifield), ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya timu hizo mbili kuelekea kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.

Akiongea na wanahabari kuelekea mchezo huo, Jesus amesema, ''Najisikia vizuri ila ni jukumu kubwa sana nitajitahidi kuhakikisha naitetea nchi yangu, nimeshaongea na baadhi ya wachezaji wamenitania sana lakini wameniahidi ushirikiano''.

Kwenye fainali za Kombe la Dunia, Brazil ipo kundi E na timu za Costa Rica, Switzerland na Serbia. Itacheza mchezo wake wa kwanza Juni 17 dhidi ya Switzerland. Timu hiyo pia ndio mabingwa wa historia wa kombe hilo wakiwa wamelitwaa mara tano.

No comments

Powered by Blogger.