Full-Width Version (true/false)


Jeshi lilivyokatisha ndoto za Dkt. Kijo-BisimbaMkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), ambaye amebakiza muda mchache kumaliza muda wake katika kutumikia LHRC, Dkt. Helen Kijo-Bisimba amefunguka na kudai mfumo wa elimu wa zamani ulipoteza ndoto zake za kutaka kwenda kusoma chuo Kikuu moja kwa moja. 
Dkt. Kijo-Bisimba ametoa siri hiyo ya maisha yake wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha East Africa Drive inayorushwa na East Africa Radio na kusema kilichopelekea kutokea hayo yote mpaka kushindwa kuenda kusoma Chuo Kikuu na matokeo yake kusomea ualimu ni kutokana na mfumo wa elimu kufanyiwa mabadiliko wakati wao wamemaliza.

"Tulimaliza kusoma kidato cha sita tukijua tunaenda Jeshini kwa miezi sita halafu tuelekea Chuo Kikuu lakini tukaambiwa hapana, na kwamba sera imebadilika hivyo mnapaswa kuenda JKT miezi 12", amesema Dkt. Kijo-Bisimba.

Pamoja na hayo, Dkt. Kijo-Bisimba ameendelea kwa kusema "kabla ya hapo walikuwa hawajajipanga vizuri tukajikuta miezi sita ya awali tumekaa nyumbani tu, hatujui ni lini tutaenda Jeshini ambapo tulimaliza shule Novemba 1974 na tukakaa mpaka Julai 1975 ndipo tulipoweza kwenda Jeshini".

Msikilize hapa chini Dkt. Helen Kijo-Bisimba akiendelea kusimulia stori nzima ya maisha yake kuhusiana na sakata la elimu lilivyoweza kumtokea kipindi anamaliza kusoma kidato cha sita mnamo mwaka 1974.

No comments

Powered by Blogger.