Full-Width Version (true/false)


Jezi za Simba, Yanga zatawala Fainali ya FA

  

Mchezo wa fainali baina ya Mtibwa Sugar na Singida United umekua neema kwa wauza jezi wa timu ya Simba na Yanga kuliko hata za timu husika. 

Wauza jezi walianza kutua uwanjani mapema huku wakiwa na mafurushi ya jezi hasa za mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba ambayo kwa sasa wapo Nairobi kwenye michuano ya SportPesa Supercup. 

Mmoja wa wauza jezi Saidi Michael alisema asilimia kubwa ya mashabiki huuliza jezi za timu hizo ndio maana imekuwa ngumu kwao kuuza za Mtibwa na Singida kwa sababu ya kuangalia maslahi ya biashara. 

“Sisi ni wajasiliamali ambao hatuegemei popote hivyo tunaangalia upepo wa kazi jinsi unavyokuwa ndio maana hata hapa unaona jezi chache za Singida lakini za Simba zipo Nyingi” alisema Michael. 

Aliongeza kuwa siyo jambo geni kuonekana hapa kwani mikoa mingi wanayokwenda kwenye michuano mbalimbali hasa ya ligi kuu kwa kuuza jezi za timu hizo kuliko timu wenyeji licha ya bei kutofautiana kwa kila jezi.

No comments

Powered by Blogger.