Full-Width Version (true/false)


JINSI watoto wa mitaani walivyojaaliwa vipaji


 NA ANASI SELEMANI MLANGI 0715329862 

Waswahili wanasema,Kozi mwandanda kulala na njaa kupenda !
Ya kwamba kufaulu na kufeli na kupata na kukosa juu ya jitihada zako mwenyewe. Kila kukicha Nchini janga la ongezeko la watoto wa mtaani lazidi kuongezeka.

Sitaki kusema sana sababu zinazopelekea janga hilo kuzidi kuwa gumzo kwani zimezungumzwa sana.

Takwimu za hivi karibuni kutoka wizara ya afya, maendeleo ya jamii jinsia na watoto zinaonesha kuwa janga hilo limeongezeka kwa kasi hususani katika majiji.

Kupitia shirika la Railway linalopambana na tatizo la watoto wa mitaani limebainisha mikoa ya Arusha, Dar Es Salaam, Mwanza, Iringa na Mbeya tatizo hilo limekithiri.

Utafiti huo kuwa idadi ya watototo wa mitaani nyakati za mchana wanakuwa 6343 na nyakati za usiku ni 1385 katika mikoa hiyo.

Wanasema dhahabu hung'aa gizani ndivyo hivyo nyota ya watoto wa mitaani ilivyong'aa huko Urusi.

Waswahili husema “ukiwaona ni watu moyoni hawana utu” watoto wa mitaani ni kundi ambalo dhalili mno katika katika jamii, wamekuwa wakiitwa majina kadhaa wa kadha yasiyopendeza kama vile machokoraa, vibaka, viteja na kadhalika.

Lakini tunapaswa kufahamu kuwa watoto hao wanavipaji vingi tofauti tofauti kama masubwi, mpira wa miguu, muziki, mpira wa pete, riadha, tenes na kadhalika.

Nao mbuyu ulianza kama mchicha Zlatan Ibrahmovic  na  Manny Pacquiao ni moja kati ya watu maarufu na matajiri duniani ambao wametokea katika maisha ya mazingira magumu.

Timu ya wasichana ya Tanzani inayoundwa na watotot washio katika mazingira magumu katika kituo cha TSC jiji Mwanza wameonyesha uwezo mkubwa katika kombe la la dunia Urusi la la watoto waishio katika mazingira magumu.

Tanzania imedhihirisha kuwa na vipaji vikubwa vya watotot waishio mitaani kwani mara  mfululizo achiliambali mwaka 2014 waliweza kutwaa kombe la dunia Nchini Brazil kwa kuwafunga hata mwaka huu pia wameweza kufanya vizuri kwa kuwafunga 5-0 Marekani kabla ya kuwafunga Uingereza 2-1 na kutinga fainali na kuchukua kombe la mshindi wa pili baada ya kufugwa goli 1 kwa 0 na Brazil.

Asilimia kubwa ya manguli wa kisoka na ndondi wametoka mitaani ipokuwa wa Makongo Sekondari ila hata wao pia wametoka mitaani
Eti nasikia kwamba Yule mfungaji bora wa timu ya watoto wa mitaani iliyoshonda michuano ya kombe la dunia mwaka 2014 na kutwaa taji hilo kwa sasa ni dereva pikipiki maarufu kama bodaboda.

Hii inaonesha hamna umakini katika kuendeleza vipaji vya mitaani badala yake tunazidi kulalamika hatufanyi vizuri katika tasnia ya michezo.

Usidharau usiyemjua twendeni tukatafute vipaji ili iwe sababu ya kupunguza kama sio kumaliza tatizo la watoto wa mitaani.

Hatuna budi kushitka sasa na kuthamini vipaji vilivyopo na na kuvisimamia na kutekeleza kauli ya Mh. Dkt. Rais John Pombe Magufuli tarehe 19 may 2018 pale Taifa akisema anatamani siku moja vile vipaji viendelezwe wale watoto wacheze timu ya Taifa.

Elimu ni bahari tujifunze kwa wenzetu Wajerumani njia zipi wametumia katika soka la watoto waishio mazingira magumu na kusaka vipaji katika nchi yao  

No comments

Powered by Blogger.