Full-Width Version (true/false)


JKT yawapa onyo kidato cha sitaJESHI la Kujenga Taifa (JKT) limewatahadharisha wahitimu wa kidato cha sita mwaka 2018 kuwa mwisho wa kuripoti kambini ni kesho. 

Taarifa iliyotolewa juzi na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu ya JKT, ilieleza kuwa ni kosa kisheria kwa mhitimu yeyote wa elimu ya kidato cha sita aliyeteuliwa kuhudhuria mafunzo hayo kwa mujibu wa sheria kukaidi. Katika taarifa hiyo, JKT imewakumbusha vijana wote walioteuliwa kujiunga na mafunzo hayo kwa mwaka 2018 kuwa terehe ya mwisho ya kuripoti kambini ni Juni 10, mwaka huu. 

“Mkuu wa JKT anawakaribisha vijana wote walioteuliwa waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia taifa,” alisema. Aidha, taarifa hiyo ilisema kuwa orodha kamili ya majina ya vijana, makambi ya JKT waliyopangiwa na vifaa wanavyotakiwa kuripoti navyo ipo katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz 

 Mei 24, JKT katika taarifa yake kwa vyombo vya habari ilieleza wateuliwa katika mafunzo hayo wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho waripoti kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mkoa wa Pwani kwa sababu ina miundombinu ya kuhudumia jamii hiyo na wengine katika kambi mbalimbali walizopangiwa. 

“Wahitimu wengine wamepangiwa kambi ya JKT Rwamkoma, Mara, JKT Msange, Tabora, JKT Ruvu, Pwani, JKT Makutupora, Dodoma, JKT Mafinga, Iringa, JKT Mlale, Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba, Tanga. “Wengine wamepangiwa JKT Makuyuni, Arusha, JKT Nachingwea, Lindi, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila, Kigoma,” ilieleza taarifa hiyo.

No comments

Powered by Blogger.