Full-Width Version (true/false)


Kabla ya fainali Mtibwa na Singida zina rekodi hii
Kuelekea fainali ya Kombe la Shirikisho nchini ASFC, itakayopigwa kesho kati ya Mtibwa Sugar na Singida United, timu hizo zimejiwekea rekodi ya pekee ambapo kila timu haijapoteza mchezo kwenye michuano hiyo. 
Mechi ya kesho ndio itakuwa mechi ya kwanza kwa timu kufungwa ambapo lazima mshindi apatikane hivyo timu moja itaondoka na kichapo huku nyingine ikimaliza mashindano bila kufungwa.

Singida United na Mtibwa Sugar zilianzia hatua ya 64 bora ambapo zilishinda mechi zake na kuingia hatua ya 32 ambapo pia zilishinda kabla ya kucheza robo fainali ambapo Mtibwa iliitoa Azam FC na Singida United ikaitoa Yanga.

Katika nusu fainali Singida United iliitoa JKT Tanzania na Mtibwa Sugar wakaitoa Stand United. Hata hivyo Singida United imeifikia rekodi ya Mbao FC ambayo ilipanda msimu wa kwanza na kufika fainali ya kombe hilo.

Mchezo wa fainali kesho utapigwa kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, kuanzia majira ya saa 10:00 Jioni na mshindi ataungana na Simba kuiwakilisha nchi kimataifa.

No comments

Powered by Blogger.