Full-Width Version (true/false)


Kabudi afafanua kuhusu kishika uchumba, Makinikia


 Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesema mazungumzo kati ya serikali na Kampuni ya Barrick yanaendelea vizuri na yanaweza kumalizika kati ya mwezi huu na mwezi ujao. 

Prof. Kabudi ameyasema hayo leo, alipokuwa akichangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha wa 2018/19.

"Sakata la makinikia  lilipoanza tulitishwa sana, tuliambiwa tutafilisiwa na ndiyo maana wajumbe wengine waliokuwa wakifanya yale majadiliano na wazungu walifichwa. Tangu sheria hii imeundwa hakuna makinikia mabayo yamekwenda nje ya nchi. Itakuwa ni marufuku kusafirisha  makinikia kinyume na masharti yaliyowekwa na sheria ya madini" Prof. Kabudi.
Majadiliano yanaendelea vizuri kati ya Barrick na Serkali kati ya mwisho wa mwezi June au katikati ya Julai tulipanga iwe mwisho wa majadiliano hayo ambapo ukamilikaji wake ni pamoja na utaratibu wa malipo ya dola mil 300 kwa mapenzi ya Mungu.

Pamoja na hayo "hatukuishia hapo ili kuhakikisha sekta ya madini inawanufaisha Watanzania, serikali inafanya mazungumzo na kampuni nyingine za uchimbaji wa madini zikiwamo kampuni 10 zinazojihusisha na biashara ya madini ya Tanzanite'.

Ameongeza kuwa "Kampuni ya Tanzanie One ambayo imeshaanza mazungumzo na serikali imekubali kuilipa fidia serikali kutokana na ufanyaji wake wa biashara nchini na pia kampuni hiyo imekubali kulipa tozo na kodi zote inazotakiwa kulipa, na tayari malipo ya kwanza imeshalipwa ”.

No comments

Powered by Blogger.