Full-Width Version (true/false)


Kampuni ya Ndege ya Emirates Yazindua Ndege Isiyo na Madirisha


Kampuni ya ndege ya Emirates imezindua ndege ambayo imetengezwa na madirisha bandia

Badala ya abiria kuweza kuona nje moja kwa moja, sasa watalazimika kutazama picha kutoka nje wakiwa ndani kwa kutumia kamera za fibre-optic

Emirates inasema kuwa hatua hiyo inatoa fursa ya kuondoa madirisha yote katika ndege za siku zijazo, swala litakalozifanya kuwa nyepesi na kuongeza kasi yake.

Rais wa Emirates Sir Tim Clark amesema kuwa picha hizo ni nzuri sana ikilinganishwa na picha zinazotazamwa kwa macho.

Wafanyikazi wa ndege wanatakiwa kuona nje ya ndege iwapo kuna dharura, mtaalam wa usalama wa angani Profesa Graham Braithwaite wa chuo kikuu cha Cranfield University alisema.

"Kuweza kuona nje ya ndege katika dharura ni muhimu, hususan wakati ambapo dharura ya uokoaji inafaa kutekelezwa'', alisema.

"Wahudumu wa ndege watalazimika kuona nje katika dharura , kwa mfano wakati wa moto, kabla ya kufungua mlango na kuanza uokoaji- na kitu chochote ambacho kitahitaji nguvu kufanya hivyo haitakuwa rahisi kuidhinishwa na afisa wa usalama wa angani''.

Hatahivyo maafisa wa usalama wa angani kutoka mamlak ya kudhitibi anga barani Ulaya European Aviation Safety Agency alisema: Hatuoni changamoto yoyote ambayo haiwezi kukabiliwa ili kuhakikisha kuwa kiwango cha usalama sawasawa na kile cha ndege ambayo ina madirisha ya wahudumu wa ndege.

Profesa Braithwaite alisema kwamba kizuizi kikuu katika ndege isiyo na madirisha itakuwa abiria wanavyohisi kuhusu teknolojia hiyo.

No comments

Powered by Blogger.