Full-Width Version (true/false)


Kichuya, Simba kuna siri nzito

 

Winga wa Simba, Shiza Kichuya amesema hatma yake ndani ya klabu hiyo, itajulikana baada ya michuano ya Sportpesa. 

Kauli hiyo ya Kichuya imekuja baada ya uwepo wa tetesi kwamba leo amesaini mkataba wa miaka miwili na mabingwa hao wa Tanzania Bara, kitu ambacho amekanusha na kusisitiza bado yupo huru kwa kuwa hajasaini. 

Akizungumza na mtandao wa Mwanaspoti, Kichuya anasema "Ijulikane naenda Nairobi katika mashindano ya Sportpesa nikiwa mchezaji huru, baada ya kutoka huko ndipo ninapoweza kukaa nao chini kuzungumza kama nitabaki au la." Kaimu wa Rais wa Simba, Salim Abdallah 'Try Again' alithibitisha hilo kwamba wamefanya mazungumzo na mchezaji huyo, lakini bado hajasaini mkataba mpya. 

"Ni kweli tumekutana na mchezaji huyo na kufanya mazungumzo, lakini hajasaini bado, ikiwa tayari kila kitu kitakuwa wazi," anasema Abdallah 'Try Again' . 

Kichuya anahusishwa na kutaka kujiunga na Azam baada ya matajiri hao wa Chamazi kumtegea dau la Sh70milioni, pia inadai yuko mbioni kutimikia Misri kusaka bahati ya kucheza soka la kulipwa huko.

No comments

Powered by Blogger.