Full-Width Version (true/false)


Kilichotokea fainali ya FA Arusha ni cha kushangaza,eti tuzo ya kipa bora wanasema mshindi hajapatikana

 

Ebwana hii haijawahi kutokea kabisa ndani ya Tanzania sijui kwingine kutokana na kile kilichotangazwa katika kilele cha mashindano ya Kombe la FA kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha eti zawadi ya kipa bora imekosa mshindi. 

Katika mashindano hayo yaliyomalizika rasmi leo Jumamosi na Mtibwa Sugar kutwaa ubingwa huo sambamba na kujizolea kitita cha Sh50 mil baada ya kuifunga Singida United mabao 3-2 . 

Wahusika walioongoza utoaji wa zawadi hizo, walitangaza kutoa kwa mfungaji bora wa mashindano ambaye ni Habib Kyombo wa Mbao FC aliyefunga mabao sita na katika msimu ujao ataichezea Singida United, mchezaji bora wa mashindano ni Hassan Dilunga kutoka Mtibwa Sugar na mchezaji bora wa mechi ya fainali ambaye ni Ismail Mhesa naye kutoka Mtibwa Sugar. 

Baada ya kutangaza washindi hao, walifafanua juu ya zawadi kwa kipa bora wa mashindano kuwa imeshindwa kutolewa kwa sababu imekosa mshindi. 

Kutokana na tukio hilo wadau wengi wa soka wameshangaa na kusisitiza, kipa wa Mtibwa, Benedict Tinocco ambaye aliidakia Mtibwa mechi hizo hadi wakaibuka mabingwa alistahili kupewa.

No comments

Powered by Blogger.