Full-Width Version (true/false)


Kocha Kariobangi: Simba ilibebwa na uzoefu

 

Kocha wa Kariobangi Sharks, Ottieno Collins amesema timu yake ilistahili kuiondosha Simba katika mashindano ya SportPesa Super Cup jana Jumatatu, lakini umakini mdogo wa washambuliaji wake ulichangia anguko lao. 

Mbali na hilo, Collins alisema uzoefu wa Simba hasa kwenye kukaba ndio uliwabeba na kuwapeleka hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo ambapo sasa watakutana na Kakamega Homeboys. Simba iliiondosha Sharks kwa mikwaju ya penalti 3-2 baada ya suluhu katika dakika 90. 

"Tulikuwa na nafasi nyingi za kufunga lakini hatukuzitumia vizuri. Tumejimaliza wenyewe. Naweza kusema pia uzoefu uliiweka Simba kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele, walizuia vizuri kwa muda wote," alisema Collins.

No comments

Powered by Blogger.