Full-Width Version (true/false)


Kocha Masoud Djuma akanusha kuondoka SimbaKocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma amesikitishwa na taarifa zinazoenea kwamba amefukuzwa kazi.
 

Djuma raia wa Burundi amesema amekuwa akizisikia taarifa hizo, lakini yuko mjini hapa akiendelea na kazi yake.
 

“Hakuna aliyeniambia nimefukuzwa, kama kufukuzwa pia mambo hayawezi kuwa kienyeji namna hiyo.
 

“Hivyo niko nikiendelea na kazi yangu kama kocha msaidizi wa Simba,” alisema.
 

Simba iko mjini hapa kwa ajili ya michuano ya SportPesa Super Cup ambayo inaendelea mjini hapa.
 

Simba imeingia hatua ya nusu fainali baada ya kuitoa Kariobang Sharks ya Kenya na sasa inasubiri kuwavaa Kakamega Homeboyz.

No comments

Powered by Blogger.